1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliberali wa FDP kufungua ukurasa mpya

Dreissing,Mathias/ZPR/P.Martin6 Aprili 2011

Philipp Rösler alietazamiwa kuwa na nafasi nzuri ndio alieteuliwa kugombea wadhifa wa mwenyekiti wa chama cha FDP baada ya Guido Westerwelle kutangaza kuwa hatogombea tena wadhifa huo.

https://p.dw.com/p/RFmL
Bundesgesundheitsminister Philipp Roesler (FDP) laechelt am Dienstag (05.04.11) in Berlin im Reichtagsgebaeude vor der Sitzung des Bundesvorstandes. Der FDP-Vorsitzende Guido Westerwelle hat am Wochenende seinen Rueckzug von der Parteispitze der Liberlaen angekuendigt. Foto: Oliver Lang/dapd
Waziri wa Afya wa Ujerumani, Philipp RöslerPicha: dapd

Wakuu wa chama hicho majimboni na bungeni mjini Berlin wamekubaliana hivyo na uamuzi rasmi utapitishwa kwenye mkutano mkuu wa chama hicho cha kiliberali utakaofanyika mwezi wa Mei. Nani atakaemrithi Guido Westerwelle, ni suala lililokuwa likijadiliwa siku mbili nzima na chama cha FDP ambacho ni mshirika katika serikali ya muungano ya Kansela Angela Merkel mjini Berlin. Hatimae jawabu limepatikana. Philipp Rösler anatazamiwa kukiongoza chama hicho na kukitoa kwenye janga la matatizo, baada ya Westerwelle kutangaza kuwa hatogombea tena wadhifa huo.

ARCHIV - Der FDP-Bundesvorsitzende Guido Westerwelle spricht auf einer Pressekonferenz am Montag (21.02.2011) in der Bundeszentrale der FDP in Berlin zu den Journalisten. Westerwelle tritt beim FDP-Parteitag im Mai nicht mehr für das Amt des Vorsitzenden an. Nach Informationen der Nachrichtenagentur dpa will er aber Außenminister und Vizekanzler bleiben. Westerwelle will sich noch am Sonntag (03.04.2011) vor der Presse in Berlin erklären. Foto: Jörg Carstensen dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++
Waziri wa Nje wa Ujerumani, Guido WesterwellePicha: picture alliance/dpa

Kwa hivyo, Rösler mwenye umri wa miaka 38 atakuwa mwenyekiti kijana kabisa kushika usukani wa chama hicho cha kiliberali. Yeye; hataki kufanya kila kitu vingine bali bora zaidi. Mbali na masuala ya kiuchumi, Rösler anakitaka chama cha FDP kushughulikia zaidi sekta zinazohusika na jamii na haki za raia vile vile. Amesema:

" Kuaminiwa hakumaanishi kuwa tunapaswa kupanga upya mradi wetu, bali ni kuzingatia mwongozo wetu wa kiliberali."

Rösler alie waziri wa afya wa Ujerumani, hadi sasa hakufanikiwa kutekeleza mageuzi aliyotangaza, wala hakuibuka kama kiongozi, lakini ana haiba ndani ya chama cha FDP. Mwanasiasa huyo mwenye watoto wanne na anaetoka mji wa Hannover, ameungwa mkono, kufuatia siku nzima ya majadiliano makali katika kinyanganyiro cha madaraka.

Waziri wa uchumi Rainer Brüderle na mkuu wa waakilishi wa FDP Birgit Homburger katika bunge la Berlin Bundestag, walikuwa wakiyumba. Kwa sasa, wao watabakia na nyadhifa hizo, ukiwepo uwezekano mdogo sana wa viongozi kubadilishwa. Hata hivyo, chama cha FDP kinajiamini. Katibu mkuu wa chama hicho, Christian Lindner amesema:

"Upande wa upinzani wala usiamini kuwa chama cha FDP kimedhoofika. Sisi tumeshikamana. Maadili yetu yanatupa nguvu kuwa tutafanikiwa pia kurejesha imani."

Caption Christian Lindner, Generalsekretär der FDP, aufgenommen am 27.03.2011 während der ARD-Talksendung "Anne Will" zum Thema: "Der Schwabenstreich - Schicksalswahl für Merkel?" in den Studios Berlin-Adlershof. Foto: Karlheinz Schindler
Katibu Mkuu wa chama cha FDP, Christian LindnerPicha: picture alliance/dpa

Lakini upinzani umeshakosoa kuwa FDP, hakitofanikiwa kufungua ukurasa mpya. Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani SPD, Sigmar Gabriel amesema, FDP kinafanya kosa kubwa ikiwa kinaamini kuwa tatizo lao ni viongozi tu. Miaka hii kumi au kumi na tano iliyopita, chama hicho, kisiasa kimezidi kuwa na sera kali za kibiashara zisizozingatia ustawi wa umma na Rösler ni mwakilishi wa sera hiyo.