1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Walibya waadhimisha vuguvugu la mapinduzi

16 Februari 2013

Maelfu ya watu walikusanyika katika miji miwili mikubwa nchini Libya,yaTripoli na Benghazi Ijumaa(15.02.2013)kusherehekea miaka miwili tangu kuanza kwa mapinduzi yaliyosababisha kuangushwa kwa Moammar Gaddafi.

https://p.dw.com/p/17fHr
TRIPOLI, Feb. 15, 2013 (Xinhua) -- Libyans attend a celebration for the second anniversary of the unrest that toppled former leader Muammar Gaddafi, in Martyrs' Square in the Libyan capital Tripoli, Feb. 15, 2013 (Xinhua/Hamza Turkia) XINHUA /LANDOV Keine Weitergabe an Drittverwerter.
Maadhimisho ya mwaka wa pili wa kuondolewa utawala waGaddafi mjini TripoliPicha: picture-alliance/Landov

Katikati  ya jiji  la  Tripoli, mamia  yawatu walikusanyika   katika uwanja  wa mashahidi , wakipepea  bendera  na  maputo   na kuimba  nyimbo  za  kusifu  mashahidi waliokufa  katika  mapinduzi ya Libya  wakati  magari  yakipita  mjini  wakipiga  honi.

Mjini  Benghazi, mji  wa mashariki  ambako  ulianzia  uasi , maelfu yawatu waliandamana  katika  njia  ile ileya maandamano yaliyofanyika  Februari  15 , mwaka 2012, kichocheo  ambacho kilizusha  vuguvugu  la  mapinduzi siku  mbili  baadaye.

Protesters from Bani Walid demonstrate outside Libya's national congress compound in Tripoli October 21, 2012. About 500 protesters broke into the grounds of Libya's parliament building on Sunday to demand an end to violence in Bani Walid, a former stronghold of Muammar Gaddafi that is being shelled by militiamen from a rival town. REUTERS/Ismail Zitouny (LIBYA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST) // eingestellt von se
Maandamano mjini TripoliPicha: Reuters

Waandamanaji Benghazi

Waandamanaji wa Benghazi  pia waliwasifu mashahidi , pamoja   na wale  ambao wamepotea  na  wale ambao  wamejeruhiwa  katika mzozo  ambao  ulidumu  kwa zaidi  ya miezi  minane  hadi  pale alipouwawa kanali Gaddafi  Oktoba 20, mwaka  2011. Lakini waandamanaji  pia wamekosoa  viongozi  wapya, wakidai  hususan kugawana  zaidi  madaraka.

Serikali  tayari  imechukua  hatua madhubuti  za  kudhibiti  jaribio lolote  la  waungaji  mkono  wa utawala  wazamani  kufanya fujo huku  waandamanaji  wakiwa  na  hasira  wanawashutumu  watawala wapya  kwa  kushindwa  kuleta  mabadiliko.

Baadhi  yawakosoaji wa serikali wamediriki  hata  kutoa wito  wa mapinduzi  mapya, wakati wakishutumu  madaraka ya wanamgambo wa zamani  ambao  walisaidia kufikisha  mwisho  utawala  wa kanali Gaddafi wa zaidi  ya miongo  minne.

People celebrate Libya's liberation in Misrata on Oct. 23, 2011, after the death of former leader Muammar Gaddafi. Gaddafi's body was temporarily displayed in the western Libyan city.
Sherehe mjini Tripoli kusherehekea miaka miwili tangu kuondolewa utawala waGaddafiPicha: picture-alliance/dpa

Maandamano  yafutwa

Wakati  huo huo  viongozi  wa  makundi  yanayotaka  kupata utawala wa ndani  waeneo  la  mashariki ya Libya wamefuta maandamano  yaliyopangwa  kutokana  na  hofu  za  kutokea ghasia jana  ijumaa, wakati  maelfu yawatu waliingia  mitaani  kuadhimisha miaka  miwili  tangu  kuanza  kwa  vuguvugu  la  mapinduzi  nchini humo.

Makundi  mjini  Benghazi, yanayojita , vuguvugu  la  mapinduzi  ya mwaka  2011  ambayo yalimuondoa  kanali  Gaddafi  kutoka madarakani, yalitayarisha  maandamano  makubwa kudai  usalama zaidi na uwekezaji  katika  mji  huo  wa pili  kwa ukubwa  nchini Libya.

SIRTE, LIBYAN ARAB JAMAHIRIYA: A delegate walking in a hallway of the Sirte Conference Centre observes a billboard with Libyan president Muammar Khadafi hosting the Fifth Ordinary Session of the Assembly of the African Union 03 July 2005. Preliminary and comity meetings are being held in this city 450 kilometers east of Tripoli in preparation to the two-day presidential summit expected 04 July. AFP PHOTO/CRIS BOURONCLE (Photo credit should read CRIS BOURONCLE/AFP/Getty Images)
Bango linalomwonesha dikteta GaddafiPicha: AFP/Getty Images

Hali ilikuwa  ya mchanganyiko  baina  yawale  waliokuwa wakiimba kwa furaha   na  kupunga  bendera   na  wale  waliokuwa  wakiimba wimbo  wa taifa, nyuso  zao  zilipakwarangi  ya  bendera  ya Libya, na wale  ambao  walikuwa  wamesimama  tu  wakutumbua  macho bila  kuonyesha  hisia  yoyote.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre /afpe

Mhariri: Sudi Mnette