1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliouwawa Munich wafikia 10

23 Julai 2016

Mtu aliyefanya shambulio la kigaidi la bunduki mjini Munich ni kijana wa miaka 18 Mjerumani mwenye asili ya Iran, lakini lengo la shambulio hilo halijafahamiki.

https://p.dw.com/p/1JUdM
Deutschland Olympia Einkaufszentrum in München Hauptbahnhof Großeinsatz
Polisi wa Ujerumani akiwa katika operesheni mjini MunichPicha: Getty Images/J. Simon

Mtu aliyefanya shambulio la kigaidi la bunduki mjini Munich ni kijana wa miaka 18 Mjerumani mwenye asili ya Iran, lakini lengo la shambulio hilo halijafahamiki.

Watu kumi wameuwa na wengine karibu 21 wamejeruhiwa katika shambulia la risasa katika eneo la maduka mjini Munich nchini Ujerumani, Polisi imetaja kuwa hilo ni tukio la kigaidi huku Kansela Angela Merkel akitarajiwa kuongoza baraza la taifa la usalama leo hii kufuatia mkasa huo.

Hakuna mshukiwa mwingine katika tukio hilo lilitokea katika eneo la jengo la maduka kiasi ya kilometa 5 kaskazini magharibi mwa eneo la kati la mji wa Munich.

Hali mbaya ya kigaidi

Polisi wamezungumzia kuhusu "hali mbaya ya kigaidi" katika mji huo wa kusini mwa Ujerumani baada ya mashambulizi ya risasi katika eneo la maduka la Olimpia na kusababisha polisi kuwaondoa watu kutoka katika eneo hilo na hali ya mtafaruku mkubwa katika mji huo.

Deutschland Olympia Einkaufszentrum in München Hauptbahnhof Großeinsatz
Kikosi maalum cha polisi kikijiandaa kufanya msakoPicha: picture-alliance/AP Photo/S. Widmann

Uchunguzi wa mwili wa mtu wa tisa , uliopatikana kiasi ya kilometa moja kutoka katika kituo hicho cha maduka , unaonesha alifariki katika hali ya mapambano, polisi wamesema.

Maafisa mjini Munich wamekiweka tayari kikosi cha kupambana na ugaidi cha GSG 9 na kuomba wanajeshi zaidi kuimarishwa kikosi hicho na polisi zaidi kutoka sehemu nyingine nchini humo.

Tahadhari ya habari za mitandao ya kijamii

Marcus Da Gloria Martins,msemaji wa polisi wa Munich, "Wacha tuseme hivi: ni moja kati ya changamoto kubwa kabisa kushuhudiwa katika miongo kadhaa ambayo polisi ya Munich inakabiliana nayo."

Deutschland Olympia Einkaufszentrum in München Polizeichef Andra-Adressen
Mkuu wa polisi wa Munich Andra akizungumza na waandishiPicha: Reuters/A. Wiegmann

Aidha afisa huyo wa polisi alitoa tahadhari kwa raia wa eneo la tukio, "Raia wanapaswa kuzingatia jambo moja: kuwa watulivu na waangalifu na kuwaaminii polisi, ambao wamekuwa wazuri kwa Munich. Kwa upande mwingine wasishiriki katika mambo ya dhania. Mitandao ya kijamii nayo imekuiwa tatizo kwa jambo hili. Mambo mengi yasio na taarifa ya kutosha yamekuwa yakisambazwa. Hali ya isiyoeleweka imekuwa ikiripotiwa kupitia simu zetu za dharura. Tunawashauri kujiepusha na hayo na nawashauri watuache tutekeleze jukumu letu"

Hakujakuwa na tukio lingine la kigaidi mjini Munich, polisi imesema, ikikanusha ripoti za vyombo vya habari nchini Ujerumani kwamba kulikuwa na tukio jingine la mapambano katika eneo la Karlsplatz, ambalo pia linafahamika kama Stachus, karibu na eneo la kati la mji huo na kiasi ya kilometa tano kutoka eneo la maduka la Olimpia.

Tangazo la hali ya dharura

Halmashauri ya jiji imetangaza hali ya dharura na kuwataka watu wasalie majumbani mwao, safari za treni vilevile zimesimamishwa katika kituo kikubwa cha treni cha Munich. Tukio hilo linatajwa kuwa la tatu kwa ukubwa kufanywa dhidi ya raia katika eneo la Magharibi mwa Ulaya katika kipindi cha miaka minane. Matukio ya hivi karibuni yenye kufanana na hilo ni pamoja na lile la Nice nchini Ufaransa na katika treni jimboni Bavaria ambayo yote yanadaiwa kufanywa na wafuasi wa kundi la Dola la Kiislamu.

Lakini pamoja na polisi kukiita kitendo cha mauwaji ya watu tisa kuwa cha kigaidi lakini vilevile imeongeza kuwa hakuna kiashria chochote chenye kuunganisha mkasa huo na ugaidi. Rais wa Marekani Barck Obama ameahidi kutoa ushirikiano kwa Ujerumani katika kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake kwa waliohusika.

Mkasa huo vilevile umemlazismisha Waziri wa Mambo ya ndani wa Ujerumani Thomas de Maizire kurejea nyumbani haraka wakati huohuo wataalamu wa kuchunguza miripuko kutoa Munich leo hii wanachunguza begi la kubeba mgongoni lililopatikana kwa mtuhumiwa mmoja aliyeuwawa katika mkasa huo. Mwili wake ulipatikana kilometa moja kutoka katika eneo la maduka ambapo ufyatuaji wa risasi ulifanyika. Kwa mujibu wa shirika la habari la hapa Ujerumani DPA bado polisi inawasaka watuhumiwa watatu.

Mwandishi: Sudi Mnette AFP/DPAE
Mhariri: Sekione Kitojo