1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanachama wa ETA wahukumiwa.

19 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cdn3

Madrid. Mahakama ya kupambana na ugaidi nchini Hispania imewahukumu wanachama 47 wa kundi linalotaka kujitenga kwa jimbo la Basque kwa kuhusika kwao na kundi lenye silaha la ETA. Wamehukumiwa kwenda jela kwa kati ya miaka miwili na 20.

Hukumu hizo zilitolewa kufuatia kesi kubwa kabisa nchini Hispania inayolihusu kundi la ETA ambayo imedumu kuanzia mwezi Novemba 2006 hadi March mwaka huu. Ikikabiliwa na uchaguzi mkuu mwezi March mwakani , chama cha kisoshalist cha waziri mkuu Jose Luis Rodriguez Zapatero kimechukua msimamo mkali dhidi ya ETA tangu pale kundi hilo lililoachana na makubaliano ya miezi 15 ya kusitisha mapigano Juni mwaka huu. ETA inatambulika kama kundi la kigaidi na Marekani, umoja wa Ulaya.