1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi 2 wa Ujerumani wauwawa

21 Oktoba 2008

Wanajeshi 2 wa Ujerumani pamoja na watoto 5 wauwawa Afghanistan.

https://p.dw.com/p/Fe2f
BundeswehrPicha: picture-alliance/dpa

Siku chache baada ya Bunge la Ujerumani-Bundestag kuidhinisha kurefusha muda wa kutumika majeshi ya Ujerumani nchini Afghanistan, jana wanajeshi wake 2 waliuwawa na wengine 2 wamejeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga.Hujuma hiyo ililengwa katika mlolongo wa magari ya wanajeshi hao huko Kundus,kaskazini mwa Afghanistan.Watoto 5 pia waliuwawa katika hujuma hiyo. Wapiganaji wa kiislamu wa Taliban wamechukua dhamana ya shambulio hilo.

Ishara kuwa jimbo la Kundus ni hatari mno,ziliibuka mara kwa mara na sasa kwa mara nyengine askari wa kijerumani wameuwawa.Gavana wa jimbo hilo la Kundus Mohammed Omar, amethibitisha mauaji hayo katika mazungumzo na studio ya kituo cha radio ya ARD cha kusini-mwa Asia.Asema:

"Pale askari wa kijerumani pamoja na polisi na wanajeshi wa Afghanistan walipotaka kufanya msako katika eneo walilolitilia shaka ,mtu aliejitoa mhanga aliepanda baiskeli, alijiripua karibu na mlolongo wa magari ya wanajeshi hao.Mshambulizi huyo alivaa kizbao chenye miripuko."

Kwa muujibu alivyoarifu zaidi gavana huyo wa jimbo la Kundus, watoto 5 waliokua wakicheza karibu na hapo waliuwawa pia katika hujuma hiyo.Watoto wengine na wanajeshi wengine 2 walijeruhiwa.Kwa magaidi hao hawajali raia ,imedhihirika wazi hata siku za nyuma.

Kikosi cha kimataifa cha ISAF ambacho kwa niaba yake wanajeshi wa Ujerumani wanatumika Afghanistan ,kimethibitisha pia kuuwawa huko kwa wanajeshi 2 wa kijerumani na wsatoto 5.Watalibani hawakukawia kujitwika dhamana ya hujuma hiyo.Katika mtandao wao ,msemaji wao aliarifu kuwa mtu aliejitoa mhanga mwenye jina Islamuddin amejiripua.Shabaha ya magaidi hao ni vikosi vya nchi za magharibi kuvihilikisha na mwishoe kuvitimua nchini Afghanistan.Ni siku chache tu nyuma ,gavana wa Kundus alipoarifu kwamba ukosefu wa kazi katika jimbo la kundus ni mkubwa mno.Na hii inasababisha kuongezeka hasira za wakaazi na hii yapelekea kuwa tayari kujitoa mhanga. Gavana wa Kundus anasema:

"Katika eneo hili kuna wapiganaji wengi wa Taliban na hata wa Alqaeda.Hii inatokana na kuwa jimbo hili lilikuwa mojawapo ya mashina yao.Watalibani wanawapa fedha wasio na kazi ili kujiripua na wanagharimia pia miripuko."

Shambulio hilo limezuka katika wilaya ile ile karibu na Kundus ambako mwishoni mwa mwezi wa August,mjerumani mwengine aliuwawa pale gari lake lilipokanyaga bomu lillozikwa.Hii iikua ishara kwamba, jimbo la Kundus na vitongoji vyake, ni hatari sana kwa wanajeshi wa nchi za magharibi. Mkuu wa kikosi cha eneo hilo Jurgen Weight wiki iliopita alieleza jimbo la kundus kuwa zamani ni shina la watalibani kaskazini mwa Afghanistan. Mafungamano yao ya zamani bado yangalipo hadi leo-alisema.

Hata miaka iliopita katika hujuma iliofanywa Kundus, waliuwawa wanajeshi 3 wa kijerumani walipokuwa njiani wakienda sokoni.Na sasa siku chache tu baada ya Bunge la Ujerumani-Bundestag kurefusha muda wa vikosi vya Ujerumani nchini Afghanistan,wanajeshi wengine wa Ujerumani wauwawa.