1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa EUROF watakawia kuwasili Tchad

Oummilkheir29 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUcu

Vienna:

Wanajeshi 4300 wa vikosi vya nchi za Ulaya nchini Tchad,EUFOR watakawia ,pengine baada ya Krismas.Sababu ya hali hiyo ni matatizo ya usafiri,-amesema msemaji wa uongozi wa EUFOR Pat Nash mjini Vienna Austria.Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Austria,nchi inayopanga kuchangia wanajeshi 160 amethibitisha shughuli za wanajeshi wa EUFOR nchini Tchad zitakawilishwa.Stefan Hirsch wa makao makuu ya EUFOR mjini Paris amezungumzia matatizo yanayobidi kutattuliwa katika shughuli za usafiri ,matibabu na wauguzi pia.Wanajeshi wa EUFOR wanaopaswa kutumikia shughuli za umoja wa mataifa nchini Tchad walikuwa waanze shughuli zao za kuwalinda wakimbizi wa Darfour nchini Tchad mwezi huu unaomalizika wa November.