1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi waasi Madagascar

18 Novemba 2010

Wanajeshi waliotekeleza uasi kisiwani Madagascar na kudai kwamba wamechukua madaraka ya nchi hiyo, wanasemekana wako katika kambi zao na wameanzisha mazungumzo na serikali.

https://p.dw.com/p/QCJy
Mwanajeshi jijini Antananarivo
Mwanajeshi jijini AntananarivoPicha: AP

Kulingana na vyanzo vya habari mazungumzo hayo yanasemekana yasipofaulu, serikali ya Madagscar itawachukulia hatua kali wanajeshi hao na kwamba hakutakuwa na msamaha.

Mazungumzo hayo yanafanyika siku moja baada ya Generali Noel Rakotonandrasana, Waziri wa zamani wa masuala ya kijeshi nchini humo aliyehusika kwa kiasi kikubwa na mapinduzi ya Machi 2009 yaliyomleta madarakani Andry Rajoelina, kutangaza kwamba taasisi zote za serikali zimesimamishwa na kwamba baraza la jeshi limechukua madaraka.

Rajoelina amesema kwamba serikali itatekeleza jukumu lake na kwamba wahusika watachukuliwa hatua. Jaribio hilo la mapinduzi lilifanyika wakati raia nchini Madagascar walikuwa wanaipigia kura ya maoni katiba mpya.