1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi walioasi serikali wasakwa Syria

22 Novemba 2011

Wanaharakati mjini Beirut wamesema majeshi nchini Syria yalivamia maeneo kadhaa ya mji mkuu Damascus wakiwasaka wanajeshi walioasi

https://p.dw.com/p/13EnQ
Vifaru vya jeshi nchini SyriaPicha: AP Photo / SHAMSNN

Huku wanajeshi hao wakiendelea na harakati zao za kuwasaka wanajeshi walioasi, milio ya risasi ilisikika katika eneo la Douma karibu sana na mji mkuu Damascus. Omar Iidibi mwanaharakati nchini Syria amesema majeshi yanayomtii rais   Bashar al-Assad yalionekana yakiwasili katika eneo hilo kwa basi.

Hatua hii imekuja saa chache baada ya ujumbe wa syria kwa umoja wa mataifa unaoongozwa na Bashar al-Jaafari, kuweka wazi maazimio yaliyotolewa na Ujerumani kwa kamati ya kutetea haki za kibinaadamu ambayo inalaani vikali ghasia za miezi minane mfululizo kwa waandamanaji, zilizosababisha vifo vya watu elfu 3,500.

Syria imekuwa ikipata shinikizo kutoka kwa mataifa ya kiarabu na kimataifa kusitisha mapigano nchini humo.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, William Hague, amesema ni lazima rais Assad aondoke ili amani ipatikane Syria.

Naye waziri mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ameonya Syria kuwa iwapo itaendelea kutumia nguvu na silaha kamwe hakutapatikana utawala bora.

Hata hivyo balozi wa Syria kwenye umoja wa mataifa ameishutumu Uingereza, Ufaransa, na Ujerumani kwa kutangaza vita vya kisiasa na kidiplomasia dhidi ya nchi hiyo kwa kuunga mkono azimio la umoja wa mataifa la kulaani unyanyasaji wa haki za kibinaadam unaofanyiwa waandamanaji.

William Hague Außenminister Großbritannien
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William HaguePicha: AP

Balozi  Bashar Ja'afari amesema haya katika mkutano wa kamati ya kutetea haki za kibinaadam baada ya Balozi wa Ujeruman, Peter Wittig kuwasilisha azimio hilo.

Baraza hilo linatarajiwa kupiga kura ya kukubali azimio hii leo.  

Mwandishi Amina Abubakar/DPA/APE

Mhariri Josephat Charo