1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wapambana nchini Cote d'Ivoire

Admin.WagnerD21 Aprili 2011

Vyanzo vya kijeshi vinasema wapiganaji waliofanikisha ukombozi wa Cote d'Ivoire na kufanikisha kuingia madarakani kwa kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia na wananchi wamegeukiana na kuanza kupambana wenyewe kwa wenyewe.

https://p.dw.com/p/111lM
Wanajeshi wa Cote d'Ivoire wakijandaaPicha: AP

Wakazi wanasema mashambulizi ya silaha nzito nzito yalitanda katika mji wa Abobo hapo jana karibu na makao makuu ya mbabe wa kivita Ibrahim Coulibaly.

Vyanzo vya kijeshi vimethibitisha kwamba jeshi jipya linaloongozwa na muasi wa zamani, Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi, Guillaume Soro walishambulia makao makuu ya Coulibaly lakini walikutana na kipingamizi kikali katika mapambano yaliyodumu kwa zaidi saa moja.

Mapambano hayo yanatokea siku tisa baada ya kukamatwa Laurent Gbagbo ambaye alikaidi kuachia madaraka baada ya kushindwa uchaguzi na kubakia katika mji mkuu wa kibiashara wa Abidjan.

Mapigano hayo yanatokea katika jitihada za jeshi la Cote d'Ivoire kujaribu kuondoa wanaomuunga mkono Gbagbo, na kurejesha matumaini haraka kwa wananchi, kuimarisha usalama na kustawisha uchumi baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kuwania madaraka.

Ibrahim Coulibaly alizungumza kwa njia ya simu na Shirika la Habari la Uingereza la Reuters na kusema jeshi la nchi hiyo limeshambulia maeneo ya Abobo na Ayaman kwa tuhuma za kulisadia jeshi la Gbagbo.

Jeshi lenye askari 500 lilijiunga na jeshi la Cote d'Voire, kutoka katika hatua ya vikundi mbalimbali vya waasi vilivyoshiriki vita vya wenyewe kwa wenyewe vya 2002 vilivyokusudia kumng'oa Gbagbo.

Coulibaly amesema amekuwa mtiifu kwa rais Alassane Ouattara na kupuuza taarifa zinazoeleza kwamba vikosi vyake vimeasi baada ya mkwaruzano wa muda mrefu kati yake na jeshi jipya.

Chanzo cha habari kilicho karibu na jeshi jipya la Cote d'Ivoire kinasema mapambano yaliyotokea yanatokana na baadhi ya vikosi vya Coulibaly kutotekeleza wito wa kujiunga na jeshi la taifa la nchi hiyo.

Mkazi mmoja wa Abobo, Tiemoko Souala akizungumza kwa njia ya simu na shirika la hbari la Reuters alisema alisikia vishindo vikubwa vya mashambulizi ya makombora katika mji huo.

Mwengine Amara Toure amesema hawakuweza kutoka nje wakati wa mapigano kutokana na hofu, walikuwa wakisikia sauti za magari yakiranda randa huku na huko.

Mapigano yalitokea pia katika magharibi mwa Yopougon, ambapo jeshi la Cote d'Ivoire lilifanya mashambulizi kwa wanaoumuunga mkono Gbagbo.

Mapigano hayo yametokea wakati ambapo baadhi ya wakazi katika maeneo kadhaa nchini humo wakirejea katika maisha yao ya kawaida baada ya mapigano yaliyodumu wiki kadhaa.

Ouattara alishinda uchaguzi wa Novemba mwaka jana ambapo Gbagbo pia alidaia kashinda na kuzusha vita vya kuwania madaraka. Zaidi ya watu 1,000 walipoteza maisha na wengine zaidi ya milioni kuyakimbia makazi yao.

Mwandishi: Sudi Mnette/RTR

Mhariri:Josephat Charo