1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wauawa katika ajali ya helikopta

Martin, Prema/ ZPR20 Januari 2012

Wanajeshi 6 wa Marekani wamepoteza maisha yao katika ajali ya helikopta iliyotokea kusini ya Afghanistan. Afisa mmoja wa Marekani amesema, helikopta hiyo ilianguka katika wilaya ya Helmand.

https://p.dw.com/p/13mvZ
US Army Staff Sgt. Matthew Rodrigue, foreground, of Louisiana, from First Battalion, 502nd Infantry Regiment, 101st Airborne Division leads a platoon during a patrol in West Now Ruzi village, district Panjwai, Afghanistan's Kandahar province, Wednesday, Nov. 24, 2010.(ddp images/AP Photo/Alexander Zemlianichenko)
Wanajeshi wa Marekani wakipiga doria AfghanistanPicha: AP

Kwa mujibu wa ripoti za awali, inaaminiwa kuwa ajali hiyo sio tukio la shambulio la maadui katika eneo hilo hatari. Msemaji wa ISAF- kikosi cha kimataifa kinacholinda usalama nchini Afghanistan amesema, ajali hiyo ilitokea Alkhamisi usiku. Akasisitiza kuwa hakuna adui aliekuwepo katika eneo hilo, helikopta hiyo ilipopata ajali ajali. Hata hivyo amesema, hakuweza kutoa maelezo zaidi kwa wakati huo kwani ni vigumu kufika katika eneo la milimani. Taarifa ya ISAF imesema, sababu ya ajali hiyo inachunguzwa.