1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamazingira waonya Tanzania kuhusu kuchimba Uranium

2 Septemba 2011

Kwa mjibu wa taarifa za hivi karibuni Tanzania inaweza kuwa na ratili milioni 53 za madini ya Uranium. Kutokana na juhudi za kuyatafuta madini na vitega uchumi vya serikali.

https://p.dw.com/p/12Rx8
Vifaa vya kuchimbia madiniPicha: DW

Sekta ya madini imezidi kuwa muhimu katika uchumi wa Tanzania hata hivyo uzalishaji wa madini ya Uranium unapingwa na jumuiya ya wajerumani ya mshikamano na Tanzania.

Wanaharakati wanaotetea ulinzi wa mazingira ambao ni marafiki wa Tanzania nchini Ujerumani wamekabidhi barua kwa balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ya kupinga uzalishaji wa madini ya uranium nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa madini hayo yapo kusini na katika sehemu ya kati ya Tanzania.

Tansanias Präsident Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete wa TanzaniaPicha: DW

Jumuiya ya wa wajerumani ambao ni marafiki wa Tanzania, wanaotetea mazingira wamemwandikia barua Rais Jakaya Kikwete kupinga shughuli za uchimbaji wa madini ya Uranium nchini Tanzania. Barua hiyo iilikabidhiwa leo mjini Berlin kwa balozi wa Tanzania nchini Ujerumani.

Katika barua hiyo wanaharakati wa Ujerumani wamesema wameingiwa wasiwasi kupata habari kwamba Tanzania inashirikiana na makampuni ya kimataifa katika kuzalisha madini ya uranium. Katika barua yao wajerumani hao ambao ni marafiki wa Tanzania wamesema shughuli za uchimbaji wa madini hayo zinaambatana na hatari kubwa. Wameeleza kuwa madini ya uraniumu yanatafautiana na madini mengine kwa sababu madini ya uranium yana sumu na yanatoa miali ya hatari. Wajerumani hao marafiki wa Tanzania wamesema madini ya uranium yanaweza kutumiwa kwaa ajili ya kutengenezea silaha za nyuklia.

Wameeleza katika barua yao kwamba uchimbaji wa madini ya uraniu unayaharibu mazingira na unahatarisha afya za wafanyakazi na watu wanaoishi karibu na maeneo ya migodi.

Akifafanua sababu za kupinga uzalishaji wa madini ya uranium nchini Tanzania mwanaharakati wa mtandao wa Tanzania nchini Ujerumani bibi Ute Tim ameeleza.

Marafiki wa Tanzania nchini Ujerumani wa mtandao unaoitwa Tanzania network pia wameingiwa wasiwasi kwa sababu uchimbaji wa uranium unakusudiwa kufanyika kwenye hifadhi ya wanyama ambapo pana kiwango kikubwa cha raslimali asilia. Wamesema shughuli za uchimbaji wa madini ya uranium zinaenda kinyume na juhudi za kuzihifadhi urathi za dunia.

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Ahmada Ngemera ameahidi kuiwasilisha risala ya watu hao marafiki wa Tanzania kwa Rais Jakaya kikwete.

Mwandishi Mtullya Abdu/ Tanzania Network/Interview/Mhariri/Abdul-Rahman