1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo kunyang'anywa silaha Kongo-Kinshasa

17 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEtm

Kinshasa:

Marais wa nchi tatu za Afrika wametoa mwito kwa Wanamgambo na vikundi vyenye silaha kunyang’anywa haraka silaha zao katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Wamelaumu mauaji ya kiholela yaliyotokea hivi karibuni na kusema kuwa yanahatarisha usalama wa Kongo-Kinshasa. Rais Jose Eduardo Dos Santos wa Angola, Denis Sassou Nguesso wa Kongo-Brazaville na Omar Bongo wa Gabon, wamekutana na Rais Joseph Kabila mjini Kinshasa. Wamelaani mashambulio yaliyotokea mashariki mwa DRC na kusababisha Wanavijiji 30 kuchomwa moto mpaka kufa juma lililopita. Wamerudia mwito wao wa kwanza kunyang’anywa silaha kwa nguvu vikundi vyenye silaha kama vile ilivyokubaliwa na Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika mwezi wa Januari mwaka huu. Vita vya miaka mitano, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, vimemalizika rasmi mwaka wa juzi.