1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo wa Kipalestina washambulia wanajeshi wa Israel

6 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DJiH

GAZA:

Mwanajeshi mmoja wa Kiisraeli ameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa baada ya kushambuliwa na wanamgambo wa Kipalestina kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.Mashahidi wamesema gari la wanajeshi hao waliokuwa wakipiga doria lilishika moto kufuatia mripuko mkubwa.Helikopta na magari mengine ya jeshi yalaiyokimbilia eneo la mripuko,yalishambuliwa pia.Kundi la wanamgambo la Islamic Jihad limedai kuwa ndio lililohusika.Hata chama cha Hamas kimesema kimeshiriki katika shambulizo hilo.

Tukio hilo limezusha uwezekano wa kuzuka kwa machafuko mapya katika Ukanda wa Gaza,siku mbili tu baada ya Israel kusitisha mashambulizi yaliyoua zaidi ya Wapalestina 120.