1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo wateka zaidi ya watu 110 nchini Mali

Lilian Mtono
22 Aprili 2024

Watu wanaodhaniwa kuwa wanamgambo wa siasa kali katikati mwa Mali wanawashikilia zaidi ya raia 110 waliowateka siku sita zilizopita.

https://p.dw.com/p/4f3rY
Mali Timbuktu
Eneo la Timbuktu nchini MaliPicha: picture-alliance/AP Photo/B. Ahmed

Watu wanaodhaniwa kuwa wanamgambo wa siasa kali katikati mwa Mali wanawashikilia zaidi ya raia 110 waliowateka siku sita zilizopita, zimesema duru za eneo hilo zilipozungumza na shirika la habari la AFP.

Wanamgambo hao waliyasimamisha mabasi matatu yaliyokuwa yamewabeba raia mnamo Aprili 16 na kuyalazimisha kuelekea katika msitu ulioko kati ya Bandiagara na Bankass, afisa mmoja wa kuchaguliwa na makundi kwenye eneo hilo yalisema. Niger, Mali, Burkina Faso zaunda kikosi cha pamoja kupambana na uasi

Afisa huyo kutoka Bandiagara ambaye hakutaka kutambulishwa kwa ajili ya usalama amesema mabasi matatu pamoja na zaidi ya abiria 120 bado wanashikiliwa na wanamgambo hao.

Mali imegubikwa na makundi mbalimbali yenye mafungamano na makundi ya kigaidi ya Al-Qaeda na kundi linalojiita Dola la Kiislamu, pamoja na vikosi vilivyojitangaza kujilinda na wahalifu.