1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanawake sasa nao wabeba dhamana ya matumizi

14 Juni 2011

Kwa miaka mingi, jamii zetu zilizoea kumuona mwanamme kuwa ndiye pekee mwenye jukumu la kuongoza na kusimamia gharama za uendeshaji mambo ama akiwa kwenye mahusiano ya kawaida na mwanamke au wakiwa katika ndoa.

https://p.dw.com/p/RTO7
Wanawake wakiandamana mjini Kampala dhidi ya hali ngumu ya maisha
Wanawake wakiandamana mjini Kampala dhidi ya hali ngumu ya maishaPicha: DW

Lakini sasa, mabadiliko na mwenendo wa mambo duniani umeanza kubadilisha taswira hiyo. Na misamiati kama vile "golikipa" ambayo ilitumika kuwaelezea wanawake majumbani wanaosubiri kuchumiwa na kuletewa kila kitu na wanaume, inaanza kupotea au kuwa na maana tafauti, maana kuna wanawake wengi ambao wenyewe ni "wachezaji" na wao ndio hulisha badala ya kulishwa.

Ndiyo mada katika kipindi hiki cha Vijana Mchakamchaka, ambapo Maryam Dodo Abdullah anazungumzia hali halisi ilivyo sasa, hasa miongoni mwa vijana.

Mtayarishaji/Msimulizi: Maryam Dodo Abdullah
Mhariri: Othman Miraji