1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanawake waathiriwa zaidi na Ukimwi

Suzanne Krause / Maja Dreyer29 Novemba 2007

Inabidi kubadilisha kabisa mbinu katika kupambana na ukimwi. Haya wanayasema wachunguzi wa shirika la Umoja wa Mataifa wanaoandaa ripoti juu ya hali ya wanawake kuhusu ukimwi.

https://p.dw.com/p/CUX9
Mgonjwa wa Ukimwi nchini Afrika Kusini
Mgonjwa wa Ukimwi nchini Afrika KusiniPicha: picture-alliance / dpa/dpaweb

Idadi ya watu walioambukizwa na virusi vya ukimwi duniani kote inakaridiwa kufika Millioni 37.5. Lakini kinyume na miaka kumi iliyopita ambapo wengi wa walioambukizwa walikuwa wanaume, leo kati ya wagonjwa wawili, mmoja ni mwanamke. Tena, wale wanaoambukizwa upya hasa ni wanawake, kama anavyosema Profesa Vimh-Kim Nguyen ambaye ni kutoka chuo kikuu cha Montreal, Canada na mtaalamu wa masuala ya ukimwi: “Kwenye mkutano wetu wa hivi karibuni tulipewa takwimu mpya kuhusu maambukizi mapya kwa vijana wa Afrika Kusini. Kati ya vijana tisa mmoja ni mvulana na wengine wasichana.”


Bado lakini wataalamu wa Umoja wa Mataifa hawana ujuzi mwingi juu ya athari kwa wanawake na vilevile hawana mbinu maalum ya kuwasaidia na kuwalinda wanawake. Wanachoweza kusema lakini ni kwamba mbinu zinazotumika hadi sasa kupunguza kuenea kwa maradhi ya ukimwi hazitoshi.

Bi Nguyen anatoa mfano: “Kwa muda wa miaka mingi, katika shughuli za kuwajulisha watu juu ya ukimwi, tulijaribu kuwafundisha wanawake na wanaume kutumia mipira. Lakini ikiwa mwanamke amelazimishwa au kubakwa haimsaidii chochote kujua vipi kutumia mpira. Tumetumia sasa msimamo wa nchi za magharibi katika suala hili na hatukufahamu kwamba watu fulani mara nyingine hawawezi kujikinga.”


Profesa Vinh-Kim Nyugen anakumbusha kwamba katika nchi nyingi duniani wanawake au wasichana hawana usemi katika mambo ya kujamiiana. Wengi hulazimishwa, pia ndoa inaweza kuwa ni ya kulazimishwa.

Mtaalamu mwingine anayeshiriki kuandaa ripoti hii mpya ya Umoja wa Mataifa ni Bi Jennifer Klot wa idara ya utafiti wa sayansi za kijamii ya mjini New York, Marekani. Yeye anakosoa kwamba:´“Kampeni nyingi bado zinalenga makundi fulani kama makahaba au madereva wa malori. Lakini siku hizi, wanaoathirika zaidi kuambukizwa ni wanawake walioolewa. Sababu ni kwamba hawana usemi juu ya waume zao kujua wanafanya mapenzi na nani. Inawezakana wanafahamu vizuri tu hatari ya kuambukizwa ukimwi, lakini hawawezi kuwazuia waume zao kutembea nje ya ndoa.”


Katika ripoti yao wanaoiandika hivi sasa kwa ajili ya shirika la UNESCO wataalamu hao wa wili wanadai mbinu ya kupambana na maradhi ya ukimwi ibadilishwe kabisa. Inabidi kuwa na suluhisho linalozingatia kipindi kirefu. Pia lazima sera zibadilishwe. Bi Nyugen anakumbusha pia kwamba katika nchi nyingi watu wanataka kuambukizwa ukimwi kwa sababu kama wagonjwa wataweza kupata huduma za afya, watoto wao watalipiwa karo za shule na familia itapata msaada wa chakula. Hayo yote ni kupitia miradi fulani ya kuwasaidia walioambukizwa ukimwi. Maradhi ya ukimwi yasitumiwe kwa sera za dharura tu, bali tutambue kwamba virusi hivyo vitakaa nasi duniani kote na wakati wote, anasema Profesa Nguyen. Ripoti anayoindaa pamoja na mwenzake Bi Klot inatarajiwa kuchapisha mwanzoni mwa mwaka ujao, 2008.