1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanigeria wengi wajitokeza kupiga kura

16 Aprili 2011

Idadi kubwa ya Wanigeria wamejitokeza kupiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo hii leo, wiki moja baada ya kufanyika uchaguzi wa wabunge.

https://p.dw.com/p/10unI
Wanigeria wakisubiri kupiga kura kumchagua rais waoPicha: DW

Rais Goodluck Jonathan anapewa nafasi kubwa ya kumshinda mpinzani wake mkubwa, Muhammadu Buhari, kiongozi wa zamani wa kijeshi.

Mashambulio mawili ya mabomu yaliwatia hofu wapiga kura kwenye mji wa Maiduguri uliopo kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo, lakini utaratibu wa kuanza kwa uchaguzi uliendelea kama kawaida.

Uchaguzi wa rais miaka minne iliyopita uligubikwa na vurugu, wizi na udanganyifu. Zaidi ya watu milioni 73 wamejiandikisha kupiga kura katika vituo 120,000 vya kupigia kura nchini humo.

Nigeria ni taifa lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika likiwa na watu milioni 150 na taifa kubwa barani humo linalosafirisha nje mafuta.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo (Alle+Deu14)
Mhariri: Sekione Kitojo