1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanyarwanda 'ni wafungwa katika nchi yao': Rusesabagina

1 Julai 2023

Mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rwanda Paul Rusesabagina, ambaye alifahamika kimataifa kwa juhudi zake za kuwaokoa watu wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994, amesema kuwa Wanyarwanda ni wafungwa ndani ya nchi yao.

https://p.dw.com/p/4TIx8
Ruanda Paul Rusesabagina
Picha: Imago Images/Belga/M. Maeterlinck

Mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rwanda Paul Rusesabagina, ambaye alifahamika kimataifa kwa juhudi zake za kuwaokoa watu wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994, amesema kuwa Wanyarwanda ni wafungwa ndani ya nchi yao.

Soma pia: Rusesabagina awasili Marekani baada ya kuachiwa huru Rwanda

Katika ujumbe wa wake wa hadharani tangu alipoachiliwa huru mwezi Machi baada ya  kukaa gerezani kwa zaidi ya siku 900 nchini Rwanda, Rusesabagina aliishukuru Marekani kwa kushughulikia kuwachiliwa kwake kutoka kile alichokitaja kama "kuzimu".

Akizungumza kutoka nyumbani kwake mjini San Antonio, katika jimbo la Texas Marekani, Rusesabagina mwenye umri wa miaka 69 amesema kuwa kwa bahati mbaya hii leo, miaka 61 baadae, Wanyarwanda bado hawako huru.

Amesema Rwanda ni serikali ya kimabavu ambayo haina haki kwa raia wake na haivumilii upinzani kutoka kwa raia wake. Serikali ya Kigali iliibatilisha kifungo chake cha miaka 25 jela kwa mashitaka ya ugaidi.