1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waokozi waendelea na shughuli za misaada

20 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CJVn

Nchini Banglaesh waokozi wanaendelea na shughuli ya kuwafikishia misaada mamia kwa maelfu ya watu walionusurika na kimbunga cha wiki iliopita.

Helikopta zimekuwa zikisafirisha misaada kwa baadhi ya maeneo yalioko mbali kabisa yalioathiriwa na kimbunga hicho cha Sidr. Idadi ya vifo inatajwa rasmi kuwa watu 3,100 lakini inatagemewa kuongezeka.Chama cha Hilali Nyekundu kimesema watu zaidi ya 10,000 huenda kuwa wameuwawa kutokana na kimbunga hicho.

Kuna hofu kwamba hali ya mazingira machafu kiafya iliosababishwa na kimbunga hicho inaweza kueneza magonjwa.

Serikali ya Ujerumani imetangaza kwamba inaongeza maradufu msaada wake wa dharura kwa Bangladesh kufikia euro milioni moja.