1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalastina wapigana Gaza

Omara Mutasa14 Mei 2007

Zaidi ya watu 50 wamefariki tangu machafuko ya wapalastina yalipoanza upya ijumaa iliyopita

https://p.dw.com/p/CHES
Waziri mkuu Ismael Hanniya
Waziri mkuu Ismael HanniyaPicha: AP

Mapigano baina ya wafuasi wa chama cha Hamas na wale wa Fatah katika Mamlaka ya wapalastina yameripotiwa kuendelea leo, licha ya pande zote mbili kukubaliana pawepo usitishaji wa mapigano.

Zaidi ya watu 50 wamefariki tangu mapigano hayo kuanza ijuma ilipota.

Mapigano yameripuka tena leo baina ya makundi ya Wafasi wa chama cha Fatah na wale wa chama cha Hamas ambapo walinzi wawili wa chama cha Fatah wameuawa.

Mapigano haya mepya yametokea baada ya viongozi wa pande zote mbili kukubaliana kua usitishaji wa mapigano ungeanza saa 6:30 jana usiku .

Hii imepelekea idadi ya watu waliowawa katika mji wa Gaza kufikia 6 na wengine 30 kujeruhiwa vibaya, tangu Jana alipouwawa kiongozi moja wa chama cha Fatah na dereva wake katika mji wa Beit Lahiya, kaskazini mwa Gaza.

Msemaji wa chama cha Fatah, Abdulkarim Awad

amekilaumu chama cha Hamas kwa kuanzisha tena uhasama huo, wafasi wa chama hicho kuanza kufyétua risasi ,kuwauwa na kuwatekanyara walinzi wa Fatah.

Nae msemaji wa kundi la Hamas , Ayman Taha alisema jana usiku, wamekubali kusitisha mapigano na kuwaondoa wapiganaji wao Barabarani, na pia kuwaachia mateka wote.

Kundi la Hamas nalo linadai wanachama wake waliokamatwa na kundi la Fatah nao waachiwe huru.

Chama cha waandishi wa Habari wa palastina kimesema mwaandishi moja Suleiman Al-Asha, mfuasi wa chama cha Hamas , aliuwawa katika mapigano hayo.

Chama hicho cha waandishi wa Habari wa kipalastina kimeyalaani mauaji hayo na kutaka wote waliohusika wakamatwe.

Licha ya ahadi za mara kwa mara za viongozi wa palastina ; Rais Mahmoud Abbas wa chama cha Fatah na waziri mkuu Ismail Hania wa Hamas, kutaka pawepo weko amani na utulivu katika palastina lakini mipango ya usalama na utengamano wa sheria, imeshindwa kufua dafu huku koo za kipalastina zikiendelea kupigana.

Mwezi March makundi haya mawili Hamas na Fatah walisaini mkataba wa kuunda serakali ya pamoja katika mkutano wa suluhu uloitishwa na Mfalme Abdullah bin Abdulaziz wa Saudia Arabia .