1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapanga njama za mauji wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi wapatikana na hatia

Jane Nyingi17 Agosti 2007

Aliyekuwa waziri katika wizara ya polisi nchini Africa kusini wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi Adriaan Vlok pamoja na aliyekuwa mkuu wa polisi Johan Van Der Merwe wamehukumiwa kifungo cha nje cha miaka kumi kwa kukiri kupanga njama za kumuua mwanaharakati aliyekuwa akipinga ubaguzi wa rangi. Maafisa wengine watatu wa polisi wakati wa utawala huo pia walihukumiwa kifungo cha nje cha miaka mitano kila mmoja na mahakama mmoja mjini Pretoria

https://p.dw.com/p/CB1x

Wakiwa wamebeba mabango yeye maandishi ubaguzi wa rangi ni uhalifu dhidi ya bindamu waandamaji waliokuwa wamefurika nje ya mahakama mkuu mjini pretoria walitaka Vlok kushtakiwa kwa makosa mengine aliyoyatekeleza alipokuwa waziri katika wizara ya polisi wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi.

Vlok pamoja na wenzake walikiri kuwa walijaribu kumuua kasisi Frank Chikane kwa kutia sumu kweye chupi yake hali iliyosamsababisha kupatwa na tatizo la mfumo wa neva na kukabiliwa na ugonjwa wa akili.Kwa sasa Kasisi Chikane ni mshauri wa rais wa Africa kusini Thabo mbeki

Mwendesha mashtaka Anton Ackermann hata hiyo alisema aumuzi uliotolewa haupaswi kuchukuliwa kama ulipizaji kisasi. Ackermann aliimbia mahakama kuwa ombi la msamaha lilipatikana ambapo madai ya njama za kuua yaliondolewa.

Waziri huyo wa wizara ya polisi wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi Adriaan Vlok mwaka jana aliosha miguu ya kasisi Chikane katika hatua ya kujutia yale aliyoyatenda na kuomba toba.Baada ya kutolewa kwa humu hiyo Vlok aliuzumguzia umati wa watu uliokuwa nje ya mahakama

Chikane ambaye alikuwa mahakamani wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo alisema anataraji uamuzi huo uataleta maridhiano nchini Africa kusini badala ya kufufua uadui wa zamani.

Na matamshi yake punde tu baada ya kuondoka mahakamani yalikuwa haya....

"Hakuna yeyote katika serikali hii anataka kuwaadhibu watu au kumtesa yeyote. Tunataka amani lakini kwanza lazima tusahau ya kale ili tuweze kufanya hivyo"

Jaribio la kuumua Kasisi Chikane lilifanywa wakati alipokuwa kati mkuu wa baraza la makanisa nchini Africa Kusini. Vlok na Van der Merwe walikuwa wanahusika na usalama na utulivu nchini africa kusini katika mwisho wa miaka 1980 wakati ambapo sheria za dharura ziliwapa ruhusa kuwatia mbaroni na kuwazuia wanaharakati waliokuwa wakipinga ubaguzi wa rangi.

Tume ya ukweli na maridhinao iliyobuniwa punde tu baada ya kualizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi iliyoongozwa na mshindi wa tuzo la nobel askofu mkuu Desmond Tutu iliyachunguza makosa yote yaliyotekelezwa wakati huo na kuwapa msahama wale waliokiri kuhusika na makosa hayo.

Vlok alifika mbele ya tume hiyo na kupokea msamaha kwa kuhusika katika misusuru kadhaa ya mabomu lakini hakuomba msamaha kwa kosa la kujaribu kumuua kasisi Chikane.

Mapema mwezi huu aliyekuwa rais wa africa kusini Fw De Klerk alikanusha kuhusika katika uhalifu wowote au ukiukaji wa haki za bindamu wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi. Katika mkutano na wanahabari mjini Capetown kabla ya hukumu ya Vlok alisema kuwa amehusishwa kimakosa katika jaribio la kumuua kasisi Chikane.