1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiga kura wachagua serikali mpya Ugiriki

P.Martin16 Septemba 2007

Kiasi ya Wagiriki milioni 10 hii leo wanapiga kura kuchagua bunge jipya.Uchaguzi huu uliitishwa mapema na Waziri Mkuu Costas Karamanlis mwanzoni mwa mwezi wa Agosti,wakati ambapo chama chake cha kihafidhina „New Democracy Party“ kilikuwa kikiongoza.

https://p.dw.com/p/CH8A
Wafuasi wa Waziri Mkuu Costas Karamanlis wakibeba bendera yenye nembo ya chama chake New Democracy
Wafuasi wa Waziri Mkuu Costas Karamanlis wakibeba bendera yenye nembo ya chama chake New DemocracyPicha: AP

Lakini uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa uchaguzi wa leo utakuwa mchuano mkali kati ya serikali na chama cha upinzani cha wasoshalisti PASOK,baada ya serikali kulaumiwa uongozi mbaya wakati wa maafa ya moto hivi karibuni.

Kwa mara ya kwanza tangu kungólewa kwa utawala wa kijeshi mwaka 1974,safari hii chama chenye sera kali za mrengo wa kulia kina nafasi ya kuingia katika bunge la Athens lililo na viti 300.