1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiga kura wanakwenda kupiga kura leo.

27 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CgZi

Nairobi. Wapiga kura nchini Kenya wanapiga kura leo kuamua kuhusu nani atakuwa rais wa nchi hiyo, baina ya rais wa sasa na kiongozi wa upinzani ambao wanaonekana kukaribiana sana kwa mujibu wa maoni ya wapiga kura.

Mwai Kibaki mwenye umri wa miaka 76 anawania kuchaguliwa kwa kipindi cha pili, akijivunia mafanikio ya uchumi imara pamoja na amani nchini humo, wakati kiongozi wa upinzani Raila Odinga anataka kukalia kiti hicho ambacho kimekuwa mbali naye pamoja na baba yake kwa muda mrefu.

Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1963 nchi hiyo ilipopata uhuru kutoka Uingereza , wapigakura wa Kenya wapatao milioni 14 wanakwenda kupiga kura katika vituo 27,000 nchini humo wakiwa hawana uhakika wa nani atashinda.

Baada ya kampeni kali katika pande zote , wakati wa kuelekea uchaguzi nchini Kenya uchaguzi wa nne tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi , uliingia doa baada ya upinzani kudai kuwa kambi ya Kibaki inapanga wizi wa kura.