1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiganaji 12 wa Taliban wauwawa.

9 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZGk

Kabul. Majeshi ya kimataifa nchini Afghanistan yamewauwa takriban wapiganaji 12 wa kundi la Taliban pamoja na watoto wawili katika jaribio la kukamata ngome ya Taliban nchini humo. Maafisa wa Afghanistan wametoa wito kwa wapiganaji wa Taliban katika mji wa Musa Qala kujisalimisha, ama watakabiliana na kifo. Msemaji wa serikali ya Afghanistan amesema kuwea mamia ya raia wamekimbia kutoka mji huo baada ya kuambiwa na mapema kuhusu operesheni hiyo. Katika tukio lingine, jeshi la kimataifa la kulinda amani , limesema mmoja kati ya wanajeshi wake ameuwawa na mwingine kujeruhiwa katika mlipuko kusini mwa Afghanistan.