1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiganaji wa Arrowboys elfu saba wajisalimisha huko Uganda

13 Agosti 2007

Nchini Uganda wapiganaji wa Arrowboys elfu 7 wamejisalimisha na kurudi katika maisha ya kawaida.

https://p.dw.com/p/CH9j
Jeshi la Uganda Peoples Defence Force(UDPF) ambao wallikuwa wakipambana na wapiganaji wa Arrowboys
Jeshi la Uganda Peoples Defence Force(UDPF) ambao wallikuwa wakipambana na wapiganaji wa ArrowboysPicha: AP

Wapiganaji hao walikuwa wanapambana na jeshi la Uganda, Uganda Peoples Defence Force, UPDF katika eneo la kaskazini hususan Karamoja. Wengi ya wapiganaji hao wamejiunga na jeshi la serikali aidha polisi ili kudumisha amani na usalama. Eneo la kaskazini mwa Uganda linakabiliwa na vita vya muda mrefu vinavyoendeshwa na kundi la waasi la LRA wanaopinga serikali huku wakipambana na jeshi la UPDF. Mazungumzo ya amani ya Juba kati ya waasi hao na serikali bado hayajafua dafu.

Mwandishi wetu wa Kampala,Omar Mutasa amezungumza na Waziri Musa Ecweru aliyekuwa muasi katika kundi la UNLA hapo zamani.