1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapigania hifadhi ya hali ya hewa watunukiwa zawadi ya amani ya Nobel

12 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7GI

Oslo:

Tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka huu wanatunukiwa kwa pamoja,makamo wa zamani wa rais wa Marekani Al Gore na shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya hali ya hewa.Wanatuzwa kutokana na juhudi zao za kuwazindua walimwengu juu ya hatari inayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuelezea hatua zinazobidi kuchukuliwa.Al Gore ameshatunukiwa zawadi mbili za Oscar mwaka huu kwa filamu yake aliyoiipa jina-An Inconvient Truth” au “ukweli unaosumbua “.Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya hali ya hewa,linalowaleta pamoja wataalam elfu tatu,limegundua hivi karibuni,binaadam ndie anaebeba sehemu kubwa ya dhamana ya kuzidi hali ya ujoto duniani katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.Makamo wa zamani wa rais wa Marekani Al Gore amesema,fungu lake toka yuro milioni moja na laki moja za tuzo hiyo ya amani ya Nobel,atawatunukia wanaharakati wanaopigania hifadhi ya hali ya hewa nchini Marekani.