1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapinzani Tanzania wakatazwa kuandamana

Sudi Mnette8 Juni 2016

Polisi Tanzania imepiga marufuku maandamano na mikutano yote ya hadhara ya upinzani kwa muda usiojulikana. Upinzani uliitisha mikutano ya hadhara kwa kushinikiza kile kilichoitwa kubinywa kwa demokrasia.

https://p.dw.com/p/1J2az
Wafuasi wa CUF Tanzania
Picha: DW/M. Khelef

[No title]

Hatua hii inakuja baada ya polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi kuutawanya umati wa wafuasi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA na viongozi wao mjini Kahama, Shinyanga. Upinzani uliitisha mikutano ya hadhara nchi nzima kwa kushinikiza kile unachokieleza kubinywa kwa demokrasia kunakofanywa na utawala wa Rais John Pombe Magufuli wa taifa hilo. Kufuatia hatua hiyo DW imezungumza na msemaji wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Advera Bulimba ambaye kwanza anaelezea sababu za kuchukuliwa kwa uamuzi huo.