1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapinzani walalamika kabla ya uchaguzi Zimbabwe

29 Julai 2013

Wazimbabwe wanajiandaa kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Rais na bunge siku ya Jumatano, lakini tayari wapinzani wa rais Robert Mugabe wameshaanza kulalamika hawajapokea nakala ya orodha ya daftari la wapiga kura.

https://p.dw.com/p/19GlQ
Zimbabwe Prime Minister and leader of the opposition Movement for Democratic Change (MDC) Morgan Tsvangirai speaks at a news conference in Harare, June 13, 2013. Tsvangirai on Thursday rejected a plan by President Robert Mugabe to hold an election on July 31, accusing his rival of breaking the constitution and formenting a political crisis in the southern African nation. REUTERS/Philimon Bulawayo (ZIMBABWE - Tags: POLITICS ELECTIONS)
Zimbabwe Wahlen Morgan Tsvangirai 13.06.2013Picha: Reuters

Malalamiko haya yanakuja katika wakati ambapo kumekuwa na shakashaka nchini humo kwamba huenda kukafanyika mizengwe ya kulifanyia kiini macho daftari hilo kumpa ushindi Mugabe.Wakati huohuo Wazimbabwe waliokimbilia katika nchi jirani wanaendelea kumiminika nchini mwao kwa ajili ya kushiriki zoezi hilo.

Mwanamke akitazama bango la mgombea urais wa Mdc Morgan Tsvangirai
Mwanamke akitazama bango la mgombea urais wa Mdc Morgan TsvangiraiPicha: Reuters

Joto la kisiasa

Siku Mbili kabla ya Uchaguzi nchini humo joto la kisiasa nchini Zimbabwe limeshaanza kufukuta,kufuatia hofu ya kutokea udanganyifu.Waziri wa fedha Tendai Biti anasema chama chake cha Movement for Demokratic Change MDC kitachukuwa hatua za kisheria kuipata nakala hiyo ya daftari la wapiga kura.

Akizungumza na waandishi wa habari Tendai amedai kwamba huenda chama cha Zanu Pf ndio chama pekee kilicho na nakala hiyo ya mwisho ya orodha ya wapiga kura na mawakili wa Mdc wameshaanza mchakato wa kuwasilisha kesi mahakamani kudai kuipata nakala hiyo.Itakumbukwa kwamba mwezi uliopita shirika moja lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya utafiti lilijikita katika kuzifuatilia siasa za Zimbabwe na kuripoti kwamba daftari la wapiga kura litakalotumika katika uchaguzi huu linajumuisha kiasi majina ya watu milioni moja waliokufa au waliokimbilia nchi za nje pamoja na majina ya watu wengine laki moja wenye umri wa zaidi ya miaka 100.

Wafuasi wa rais Robert Mugabe wakimkaribisha akizunduwa manifesto yake
Wafuasi wa rais Robert Mugabe wakimkaribisha akizunduwa manifesto yakePicha: Reuters

ZEC Lawamani

Kwa mujibu wa chama cha Mdc cha waziri mkuu Morgen Tsvangirai idadi hiyo ya wapiga kura hewa inalengwa kumuongezea kura Mugabe na chama chake.Tayari Tsvangirai ameshasema haamini ikiwa uchaguzi huu utakuwa huru na wa haki

Chama cha Mdc kinanyoosha lawama dhidi ya tume ya uchaguzi kwa kutokuwa wazi katika masuala mbali mbali ikiwemo hilo la orodha ya daftari la wapiga kura pamoja na idadi ya makaratasi ya kupiga kura yaliyochapishwa.

Aidha katibu mkuu wa chama hicho Tendai Biti amesema kukamatwa kwa Morgan Komichi,afisa mkuu wa shughuli za uchaguzi za Tsvangirai ni kitendo kilichokusudiwa kuvuruga kabisa kampeini za mgombea huyo wa urais wa Mdc.Kwa hivyo chama hicho kimeonya ikiwa tume ya uchaguzi itatangaza matokeo yaliyopikwa,Mdc kitakuwa tayari kwa upande wake kutangaza matokeo yake.

Ni uchaguzi ambao bila shaka utafuatiliwa kwa karibu sio tu na wazimbabwe bali hata nje ya mipaka ya taifa hilo.Wazimbabwe wanaoishi nje wamekuwa katika harakati za kurudi nyumbani kwa ajili ya kupiga kura.Mamia wamekuwa wakivuka mpaka kutoka Afrika Kusini kuingia nyumbani,Zimbabwe.

Robert Mugabe akiwa uwanja wa michezo wa Chipazde,March 2, 2013
Robert Mugabe akiwa uwanja wa michezo wa Chipazde,March 2, 2013Picha: Reuters

Rais Mugabe aliyeingia madarakani kwanza kama waziri mkuu baada ya uhuru mwaka 1980 amewataka wafuasi wake kujitokeza kwa wingi kumrudisha tena madarakani.Rais huyo pia amewaruhusu tu waangalizi kutoka Afrika zaidi kuwaumiza mahasimu wake.

Mwandishi:Saumu Mwasimba dpa/Afpe/ZR

Mhariri :Mohammed AbdulRahman