1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapinzani watishia Senegal kutotawalika

29 Januari 2012

Upinzani nchini Senegal umetishia kufanya nchi hiyo isitawalike, endapo rais Abdoulaye Wade atashikilia kugombea wadhifa wa urais kwa muhula wa tatu katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

https://p.dw.com/p/13sVq
Senegal der Präsident Abdoulaye Wade Bild: Klaudia Pape
Rais wa Senegal Abdoulaye WadePicha: DW

Polisi mmoja aliuawa katika machafuko yaliyozuka siku ya ijumaa, baada ya  waandamanaji kuanza kurusha mawe, kupindua magari na kuchoma matairi na polisi nao walifyatua mabomu ya kutoa machozi. Mapambano hayo yalitokea baada ya mahakama kuu nchini humo kusema Rais Wade ana haki ya kuwania tena wadhifa wake kwa awamu ya tatu.

Katika hatua nyingine hapo jana polisi, ilimkamata Alioune Tine alie kiongozi wa kundi la wanaharakati wa haki za binadamu nchini humo liitwalo M23, kufuatia vurugu za ijumaa.