1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waranti kumkamata makamu wa rais wa Iraq

Martin,Prema/zpr20 Desemba 2011

Iraq imetoa waranti ya kumkamata makamu wa rais wa nchi hiyo Tareq al-Hashemi, kwa madai ya kuhusika na ugaidi.

https://p.dw.com/p/13VrO
Iraq's Sunni Arab vice president Tariq al-Hashemi speaks during a Press conference about the upcoming elections in Baghdad, Iraq, on Wednesday, Nov. 18, 2009. al-Hashemi vetoed part of a key election law, throwing national polls slated for January and a planned U.S. troop draw-down into question. (AP Photo/Karim Kadim)
Makamu wa rais wa Iraq, Tareq al-HashemiPicha: AP

Kwa mujibu wa duru za usalama na sheria, waranti hiyo imetolewa na kamati ya mahakama kuambatana na sheria za kupiga vita ugaidi. Wakati huo huo, wizara ya mambo ya ndani mjini Baghdad imesema, walinzi wa Hashemi wamekiri kupanga na kufanya mashambulio. Kwa mujibu wa ripoti ya televisheni ya Iraq, watu hao walipewa fedha na walihakikishiwa kuungwa mkono na al-Hashemi. Makamu huyo wa rais wa madhehebu ya Kisunni, ni mpinzani na mkosoaji mkali wa Waziri Mkuu Nuri al-Maliki ambae ni wa madhehebu ya Kishia.