1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Warsaw. Rais awafuta kazi mawaziri.

13 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZZ

Rais wa Poland amewafuta kazi mawaziri wanne kutoka katika vyama vidogo washirika vinavyounda muungano wa serikali. Lech Kaczynski amewafuta kazi maziri wa elimu, uchumi wa maliasili ya habari, kazi na ujenzi . Mawaziri hao wote wanatoka katika vyama vya mrengo wa kulia ama vya ulinzi wa wakulima.

Waliochukua nafasi zao wanatoka katika vyama washirika wa chama cha waziri mkuu Kaczynski cha sheria na haki.

Katika sherehe mjini Warsaw iliyohudhuriwa na ndugu yake pacha , waziri mkuu Jaroslav Kaczynski , rais huyo amesema mabadiliko hayo yanaashiria mwisho wa muungano unaounda serikali na kwamba uchaguzi wa haraka utaitishwa hivi karibuni.