1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Warsaw: Rais awatimua kazi mawaziri.

13 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZn

Rais wa Poland amewafuta kazi mawaziri wake wanne kutoka katika chama kidogo kinachounda muungano wa serikali ya nchi hiyo.
Lech Kaczynski amewafukuza kazi mawaziri wa elimu, uchumi wa maliasili ya bahari, na waziri wa kazi na ujenzi.
Wote wanatoka katika vyama vya mrengo wa kulia vya League of Polish Families ama vyama vya ulinzi wa haki za wakulima.
Nafasi za mawaziri hao zimechukuliwa na wajumbe wengine pamoja na washirika wa chama cha waziri mkuu cha Sheria na haki.
Katika sherehe zilizohudhuriwa mjini Warsaw na mdogo wake pacha wa rais huyo
ambaye ni waziri mkuu Jaroslav Kaczynski, rais amesema mabadiliko hayo yanaashiria mwisho wa muungano huo na kwamba uchaguzi wa mapema utafanyika hivi karibuni.