1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washindwa kukubaliana juu ya Kosovo

21 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CPls

Viongozi wa Serbia na wale wa asili ya Waalbania wa Kosovo wameshindwa kufikia makubaliano juu ya jimbo lililojitenga la Serbia.

Katika mazungumzo yaliofanyika hapo jana mjini Brussels Ubelgiji wasuluhishi wa Kosovo wamekataa pendekezo la Serbia la kuwa na mamlaka makubwa ya kujiamulia mambo yake yenyewe na badala yake wamesisitiza kupatiwa uhuru chini ya usimamizi wa Umoja wa Ulaya. Hata hivyo pande zote zimekubali kuendelea na mazungumzo zaidi nchini Austria wiki ijayo.

Kiongozi wa waasi wa zamani wa Waalbania wa Kosovo Hashim Thaci ambaye chama chake kimeshinda uchaguzi wa bunge wa Kosovo hapo Jumapili ametishia kujitangazia uhuru iwapo makubaliano juu ya mustakbali yatashindwa kufikiwa hapo tarehe 10 mwezi wa Desemba.