1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa ajiuzulu

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmS

Balozi wa Marekani kwa Umoja wa Mataifa John Bolton amejiuzulu.

Rais Bush amesema amekubali kujiuzulu kwa balozi huyo shingo upande na amesema kwamba hakulifurahia jambo hilo.

Akikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa chama cha Democrat ambacho hakipendezewi na mtindo na vitendo vya Bolton Bush alitumia madaraka yake ya urais kumteuwa kushika wadhifa huo hapo mwaka jana wakati bunge likiwa kwenye mapumziko ya kiangazi.

Kwa vile sasa chama cha upinzani cha Demokrat cha mrengo wa shoto wa wastani kinadhibiti mabaraza yote mawili ya bunge kufuatia uchaguzi wa mwezi uliopita yumkini kutomthibitisha kuendelea na wadhifa huo wakati kipindi chake kitakapomalizika hapo mwezi wa Januari.

Bolton mkosoaji mkubwa wa Umoja wa Mataifa na muhafidhina mashuhuri alikuwa na historia ya kuwakasirisha wanadiplomasia na wafanyakazi wenzake katika wadhifa wake wa zamani kwenye wizara ya mambo ya nje ya Marekani.