1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Baraza la Congress laidhinisha muswada wa sheria.

27 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6Y

Baraza la Congress la Marekani limeidhinisha sheria ambayo inahusisha kuondolewa kwa majeshi ya Marekani kutoka Iraq na kutoa fedha kwa ajili ya vita hivyo.Msemaji wa Ikulu ya Marekani amesema kuwa rais hatatia saini sheria hiyo ikiwa ni kusalimu amri kwa masharti hayo. Baraza la Seneti limepiga kura 51 za ndio na 46 za hapana , siku moja baada ya baraza la wawakilishi kupitisha muswada huo wa sheria ambao unatoa kiasi cha dola bilioni 100 kwa ajili ya vita vya Iraq na Afghanistan mwaka huu na wakati huo huo kuweka muda wa mwisho wa kuyaondoa majeshi ya Marekani kutoka Iraq katika muda wa miezi 11 ijayo.

Akizungumza kabla ya kupiga kura kiongozi wa kundi la Maseneti wa chama cha Democratic Seneta Harry Reid amesema kuwa kila mmoja anataka Marekani ifanikiwe katika mashariki ya kati.Ni mara ya kwanza kwa baraza lote la Congress , linalodhibitiwa na Wademocrats tangu mwezi Januari , kumpinga rais.Wakati huo huo waziri wa mambo ya kigeni wa Iraq Hoshyar Zebari ameulaumu muswada huo wa sheria, akisema kuwa unatoa ishara mbaya kwa watu wenye msimamo mkali nchini Iraq.