1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Baraza laridhia kuondolewa wanajeshi Iraq

24 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCG4

Baraza la Wawakilishi la bunge la Marekani limepiga kura kuweka siku ya mwisho ya kundolewa kwa wanajeshi wote wa Marekani kutoka Iraq ifikapo mwezi wa Septemba mwaka 2008.

Wabunge wa chama cha Demokrat wamefanikiwa kuambatanisha muda huo wa mwisho kwenye muswada unaoridhia matumizi ya zaidi ya dola bilioni 124 za mfuko wa dharura hususan kwa ajili ya vita nchini Iraq na Afghanistan kwa mwaka huu.

Ikipuuza tishio la Ikulu ya Marekani kuupigia kura ya turufu muswada huo wabunge walipiga kura 218 dhidi ya 212 wengi wao kuzingatia misimamo ya chama.

Wabunge wa chama cha Republican takriban walikuwa na sauti moja kuupinga muswada huo ambao wanasema utakuwa ni sawa na kukiri kushindwa nchini Iraq.

Baraza la Senate la bunge la Marekani linatazamiwa kuupigia kura muswada huo mapema wiki ijayo.