1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bunge la Marekani lakataa terehe ya kuondoka majeshi Irak

16 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIY

Bunge la Marekani limekataa mswada uliotaka kuwekwe tarehe ya kuwaondoa wanajeshi wa Marekani walio nchini Irak.

Chama cha Democratic kilishindwa kwa kura 50 kwa 48 na chama cha Republican kuupitisha mswada huo.

Kama ungepitishwa mswada huo ungewaamuru wanajeshi wa Marekani kuondoka Irak kufikia mwezi Machi mwaka 2008.

Rais George W Bush wa Marekani alikuwa ametishia kuutilia guu mswada huo kutumia kura yake ya turufu kama ungepata kura 60 zilizohitajika kuidhinishwa.

Mwezi uliopita baraza la wawakilishi lilipitisha azimio la kihistoria kupinga mpango wa serikali ya rais Bush kutaka kupeleka wanajeshi 21,500 zaidi kwenda Irak.