1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Bush aahidi kuendelea na mapambano dhidi ya ugaidi.

12 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtc

Rais wa Marekani George W. Bush amesema kuwa kushindwa kwa chama chake cha Republican katika uchaguzi wa baraza la Congress wiki iliyopita hakupunguzi nia yake ya kupambana na ugaidi.

Katika hotuba yake ya kila wiki kwa njia ya radio , Bush ameahidi kufanyakazi na chama cha Democrats kuhakikisha kuwa Marekani inashinda maadui zake.

Katika uchaguzi uliopita wa baraza la Congress , chama cha Democratic kimeshinda udhibiti wa mabaraza yote mawili, baraza la wawakilishi na lile la Seneti kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 12.

Wadadisi wanasema kuwa kukataa kwa wapigakura jinsi vita vya Iraq vinavyoendeshwa , ni sababu kubwa ya matokeo hayo.

Wakati huo huo rais George W. Bush anamkaribisha waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert katika Ikulu ya Marekani kesho Jumatatu, wakati chama cha upinzani cha Democratic kikidhibiti baraza la Congress na huenda kikatoa msukumo wa kufanyika mazungumzo na wale wanaoonekana kuwa maadui wa Israel Iran na Syria.

Olmert anawasili nchini Marekani wakati hali ya uongozi wa kisiasa imebadilika nchini humo.