1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Bush amsifu Dalai Lama

18 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Es

Rais George W. Bush wa Marekani akikaidi onyo la China amemkabidhi Dalai Lama hapo jana tuzo ya kiraia ya bunge yenye hadhi kubwa nchini Marekani na amewataka viongozi wa China kumkaribisha mtawa huyo Beijing na kufanya mazungumzo naye.

Bush ambaye alikutana na Dalai Lama kwa faragha hapo Ijumanne amemsifu mtawa huyo wa kibuda kuwa ni ishara ya amani na uvumilivu duniani.

Bush ni rais wa kwanza wa Marekani kuonekana hadharani akiwa pamoja na kiongozi huyo wa kidini wa Tibet anayeishi uhamishoni ambaye China inamuona kuwa ni muasi anayetaka kujitenga kwa jimbo na Tibet na ni haini.