1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Bush atakiwa kujitayarisha kwa mabadiliko ya sera.

21 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC02

Rais wa Marekani George W. Bush ameambiwa kuwa ajitayarishe kwa mageuzi nchini Uingereza kuhusiana na Iraq mara Gordon Brown atakapokuwa waziri mkuu .

Afisa katika utawala wa rais Bush hata hivyo ameieleza ripoti hiyo iliyotolewa na gazeti la Sunday Telegraph la Uingereza kuwa isiyokuwa na msingi.

Rais Bush amefahamishwa na maafisa wa Ikulu kuwa atarajie tangazo la kuondolewa kwa majeshi ya Uingereza katika muda wa siku 100 za utawala wa Brown.

Rais huyo taarifa hiyo imesema ameshauriwa jinsi ya kupambana na hali hiyo itakapotokea ya kuondolewa kwa majeshi ya Uingereza pamoja na kumalizika kwa uungwaji mkono usio na ukomo kutoka London, limesema gazeti hilo likiwanukuu maafisa waandamizi.

Waziri mkuu Tony Blair anatarajiwa kuondoka madarakani ifikapo Juni 27 baada ya kuwapo madarakani kwa muda wa muongo mmoja, na waziri wa fedha Gordon Brown anatarajiwa kuchukua nafasi yake.