1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush awataka Wamarekani kulisadia jeshi

23 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYe

Rais George W Bush wa Marekani amesema vita dhidi ya ugaidi ni mwito kwa kizazi cha sasa cha Wamarekani. Ushindi katika vita hivi ni muhimu kuhakikisha usalama na amani kwa kizazi cha kesho.

Aidha rais Bush amesema ili kuweza kulifikia hilo, Wamarekani wanahitaji kujitolea kwa dhati kulisaidia jeshi.

´Tuna jukumu la kuhakikisha jeshi letu linaweza kuendeleza vita dhidi ya ugaidi na kufanya kazi kubwa tunayotarajia ifanywe. Ninaamini tunahitaji kupanua majeshi yetu.´

Wakati huo huo, naibu kiongozi wa kundi la al-Qaeda Ayman al-Zawahiri amemkejeli rais George W Bush wa Marekani juu ya mpango wake wa kuongeza idadi ya wanajeshi nchini Irak. Kwenye ukanda wa video uliotolewa na kundi la al-Qaeda, al Zawahiri amemtaka rais Bush atume jeshi lote la Marekani nchini Irak akisema majeshi kumi ya aina hiyo yatashindwa nchini Irak.

Mapema mwezi huu rais Bush alitangaza ataongeza wanajeshi zaidi ya 20,000 nchini Irak.