1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Bush haridhishwi na hali nchini Iraq.

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmL

Rais wa Marekani George W. Bush ameeleza kutoridhishwa kwake na hali nchini Iraq, akimweleza mmoja kati ya viongozi maaruf wa kisiasa nchini humo Abdel Aziz al-hakim. Lakini Bush amesema kuwa anakubali kazi inayofanywa na al Hakim na waziri mkuu Nouri al Maliki ya kuiunganisha nchi hiyo.

Kabla ya mazungumzo hayo mjini Washington na rais Bush, al Maliki , kiongozi wa baraza kuu la mapinduzi ya Kiislamu linaloungwa mkono na Iran , kwanza alikutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice katika kile alichokieleza kuwa ni mazungumzo yaliyokuwa na uwazi. Al Hakim amesema kuwa Iraq ni lazima iwe katika nafasi ya kutatua matatizo yake yenyewe.

Nchini Iraq jana , wanajeshi wanne wa Marekani wameuwawa wakati helikopta yao ilipoanguka katika jimbo la Al-Anbar magharibi ya nchi hiyo.