1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush kubadilisha sera za kijeshi nchini Irak

22 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0F

Rais George W.Bush wa Marekani anazingatia kubadilisha mkakati wa kijeshi nchini Irak kwa sababu ya machafuko yanayozidi nchini humo.Wakati huo huo Bush katika hotuba yake ya kila juma kwenye radio alisisitiza,lengo la serikali yake ni kuwashinda waasi na kuwa na serikali nchini Irak inayoweza kujitegemea.Bush amekiri kuwa licha ya kuviimarisha vikosi katika mji mkuu wa Baghdad,kinyume na ilivyotarajiwa,machafuko hayakupunguka.Bush alishauriana na majemadari kadhaa kuhusu hali ya mambo nchini Irak.Idadi ya wanajeshi wa Kimarekani wanaouawa nchini Irak ikiongezeka,sauti zinapazwa katika Baraza la Congress na hata ndani ya chama cha Bush cha Republikan,kubadilisha sera ya vita nchini Irak.Hadi hivi sasa,idadi ya wanajeshi wa Kimarekani waliouwa mwezi huu wa Oktoba ni 70. Uchunguzi wa maoni uliofanywa Marekani,unaonyesha kuwa wapiga kura waliovunjika moyo kuhusu Irak, huenda wakahatarisha uwingi wa chama cha Republikans katika Baraza la Congress,uchaguzi wa wajumbe wa Baraza hilo utakapofanywa Novemba 7.