1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush kutangaza mkakati mpya wa Irak

12 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQT

Maafisa katika Ikulu ya Marekani wamesema,Rais George W.Bush anafanya matayrisho ya kuidhinisha mapendekezo ya kamanda wa majeshi ya Marekani, Jemadari David Petraeus kuhusu idadi ya vikosi nchini Irak.Petraeus alitoa ripoti ya kutia moyo,alipohojiwa bungeni kwa muda wa siku mbili.

Siku ya Alkhamisi,Bush anatazamiwa kutangaza mkakati wake mpya kuhusu Irak,atakapotoa hotuba yake ya taifa kwenye televisheni.