1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Bush na Merkel kutafuta suluhisho la kidiplomasia na Iran.

11 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBK4

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Marekani George W. Bush wamesema kuwa wote kwa pamoja wanafanyakazi kuelekea kupata suluhisho la kidiplomasia katika mzozo na Iran kuhusiana na mradi wake wa kinuklia.

Merkel amewaambia waandishi wa habari alipokuwa nyumbani kwa rais Bush katika jimbo la Texas, kuwa Ujerumani itaunga mkono duru nyingine ya vikwazo dhidi ya Iran iwapo nchi hiyo itaendelea kupingana na jumuiya ya kimataifa. Wakati wa ziara yake hiyo ya saa 20, Merkel ameeleza nia ya nchi yake ya kupata kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa. Kansela Merkel ameshindwa hata hivyo kupata uungwaji mkono na Marekani katika upunguzaji wa gesi zinazoharibu mazingira. Bush amesema kuwa anafahamu tatizo hilo lakini ulinzi wa mazingira hauwezi kuja kwa gharama ya kuharibu uchumi.