1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush na Olmert wamuunga mkono Abbas

19 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqD

Rais George W.Bush wa Marekani na Waziri Mkuu Ehud Olmert wa Israel wamekariri kuwa katika mgogoro wa Israel na wapalestina,wanaunga mkono suluhisho la kuwepo mataifa mawili.Viongozi hao walitamka hayo katika mkutano wao mjini Washington.Vile vile wameahidi kumsaidia Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina alieundwa serikali mpya katika Ukingo wa Magharibi.Siku ya Jumatatu, Marekani na Umoja wa Ulaya zilisema tena zinatoa msaada moja kwa moja kwa Wapalestina katika hatua ya kumuunga mkono Rais Abbas.Uamuazi huo ulipitishwa baada ya Rais Abbas wa Fatah kuivunja serikali iliyokuwa ikiongozwa na Ismail Haniyeh wa Hamas na kuunda serikali mpya ya dharura.