1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: "Chemical Ali" atauliwa hivi karibuni

19 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ed

Ali Hassan al-Majid anaejulikana pia kama „Chemical Ali“ atauliwa katika kipindi cha siku chache zijazo.Hayo alieleza msemaji wa serikali ya Iraq, Ali al Dabbagh,alipozungumza katika Ikulu ya Marekani mjini Washington.Amesema kuwa al-Majid alie binamu wa Saddam Hussein alisimamia mashambulizi ya gesi yaliyoua maelfu ya Wakurd katika mwaka 1987.

„Chemikal Ali“ mwezi Juni,alikutikana na hatia na akapewa adhabu ya kifo.Manmo mwezi wa Septemba, mahakama ya rufaa iliunga mkono adhabu hiyo.