1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Demokrat yadhidbiti baraza la wawakilishi katika uchaguzi wa bunge

8 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCur

Katika uchaguzi wa bunge la Marekani wa kipindi cha kati chama cha Democrat kimerudia tena kulidhibiti Baraza la Wawakilishi ikiwa ni miaka 12 baada ya kulipoteza baraza hilo kwa chama cha Republican.

Nancy Pelosi wa chama cha Demokrat anatarajiwa kuwa Spika wa kwanza mwanamke wa baraza hilo la bunge ambao ni wadhifa wenye nguvu kubwa kabisa katika bunge.

Akipokea habari hizo Rais George W Bush amesema matokeo hayo yanavunja moyo lakini amewahimiza wapinzani wake kushirikiana naye.

Vita vya Iraq ilikuwa ni mada kuu katika uchaguzi huo wa Marekani.

Chama cha Demokrat pia kimepata mafanikio makubwa katika jaribio lao la kutaka kudhibiti tena baraza la Senate kwa kujishindia viti vinne muhimu vya Republican vya Ohio,Pennsylavania, Rhode Island na Missouri.

Majimbo mawili bado hayakutolewa matokeo yake na iwapo Demokrat itashinda viti hivyo viwili watakuwa pia wamerudia tena kulitwaa baraza la senate.