1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Ford kuzikwa kitaifa.

28 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfd

Mazishi ya kitaifa na siku tano za maombolezi nchi nzima yanatafanyika kutoa heshima kwa rais wa zamani wa Marekani Gerald Ford. Rais wa 38 wa Marekani alifariki siku ya Jumanne nyumbani kwake katika jimbo la Califonia akiwa na umri wa miaka 93.

Mwanasiasa huyo kutoka chama cha Republican aliingia madarakani mwaka 1974 wakati alipochukua nafasi ya rais Richard Nixon, ambaye alijiuzulu kutokana na kashfa iliyojulikana kama Watergate.

Rais wa Ujerumani Horst Köhler alikuwa mmoja wa viongozi mbali mbali wa dunia ambaye alitoa rambi rambi zake, akimsifu rais Ford kuwa ni Mmarekani mzalendo ambaye amefanya kazi kubwa kuimarisha mahusiano kati ya nchi yake na mataifa ya Ulaya.