1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Gates aidhinishwa kuwa waziri wa ulinzi

6 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCm3

Robert Gates amevuka kikwazo cha kwanza kuchukuwa nafasi ya waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld.

Kamati ya huduma za kijeshi ya baraza la senate la bunge la Marekani limeidhinisha kwa kauli moja uteuzi wake huo. Akizungumza kwenye kikao cha kuthibitishwa kushika wadhifa huo Gates amewaambia wajumbe wa kamati hiyo kwamba haamini kuwa Marekani inashinda vita nchini Iraq na pia ameonya kwamba vita hivyo vinaweza kugeuka kuwa mzozo wa eneo zima la Mashariki ya Kati.

Kuteuliwa kwa Gates kwenye wadhifa huo ambaye ni mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA kutapigiwa kura na kikao kikamili cha baraza la senate baadae wiki hii.